UTURUKI
3 dk kusoma
Suluhisho la 'Zero Waste' lahitaji ushirikiano wa wengi, amesisitiza Emine Erdogan
“Licha ya kuwa na mchango mdogo sana katika mzozo wa mabadiliko ya tabianchi, Uturuki inajitahidi kwa nguvu zote kuwa sehemu ya suluhisho,” alisema mke wa Rais wa Uturuki, Emine Erdogan.
Suluhisho la 'Zero Waste' lahitaji ushirikiano wa wengi, amesisitiza Emine Erdogan
Erdogan alitangaza kwamba "hatua za lazima" zimechukuliwa ili kuanzisha ofisi ya kikanda ya UN-Habitat nchini Uturuki. / AA
tokea masaa 18

Kwa mujibu wa Mke wa Rais wa Uturuki, Emine Erdogan, ambaye pia ni mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Ngazi ya Juu la Umoja wa Mataifa kuhusu Mfumo wa Kutotupa Taka, amesema “Dunia haihitaji wachache wanaotekeleza mfumo wa kutotupa taka kwa ukamilifu, bali mamilioni ya watu wanaochukua hatua ndogo kwa uthabiti.”

Mamilioni ya wananchi wanapaswa “kubadilisha taka za nyumbani za kikaboni kuwa mbolea, kuwa na ujasiri wa kubeba chakula kilichosalia kutoka kwenye migahawa, na kuzima vifaa vya kielektroniki badala ya kuviacha kuwaka,” alisema Emine Erdogan siku ya Ijumaa katika Jukwaa la Mfumo wa Kutokuwepo kwa Taka lililofanyika Istanbul.

Pia alieleza furaha yake kwa kushiriki furaha na matumaini pamoja na washiriki wa Jukwaa la Kimataifa la Mfumo wa Kutokuwepo kwa Taka kwa mara ya kwanza.

Jukwaa hilo liliandaliwa kwa ushirikiano wa Taasisi ya Mfumo wa Kutokuwpo kwa Taka ya Uturuki, Wizara ya Mazingira, Ustawishaji Miji na Mabadiliko ya Tabianchi, Wizara ya Kilimo na Misitu, Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP), na UN-Habitat.

'Istanbul itakuwa kitovu cha ‘Zero Waste’

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo, Erdogan alitangaza kuwa "hatua muhimu" zimechukuliwa ili kuanzisha ofisi ya kikanda ya Shirika la Umoja wa Mataifa kwa Maendeleo ya Miji na Makazi Bora (UN-Habitat) huko Uturuki.

"Ninaamini kwamba, kuanzia sasa, Istanbul yetu nzuri itakuwa mji mkuu wa ‘Zero Waste’, ambapo misingi ya mustakabali endelevu itajengwa," alisema.

Aliongeza: "Mnamo 2023, tulianzisha Wakfu wa ‘Zero Waste; nchini Uturuki, kwa lengo la kuwa kitovu cha kimataifa cha mipango ya kutokuwepo kwa taka."

“Licha ya kuwa na mchango mdogo sana katika mzozo wa mabadiliko ya tabianchi, Uturuki inajitahidi kwa nguvu zote kuwa sehemu ya suluhisho,” Erdogan aliahidi.

Erdogan alihimiza ya kwamba dunia “haihitaji wachache wanaotekeleza mfumo wa kutotupa taka kwa ukamilifu, bali mamilioni ya watu wanaochukua hatua ndogo kwa uthabiti.”

Bila kuhitaji kusema, "Kama naweza kubadilisha ulimwengu," watu hawa wanapaswa "kujitahidi kufanya chochote wanachoweza, kwa uwezo wao wote, kwa manufaa ya ubinadamu," alihimiza.

Uharibifu wa mazingira unaosababishwa na vita huko Gaza

Katika Ukanda wa Gaza, kutokana na vita vya miaka miwili na mzingiro wa Israel, “uchafuzi wa udongo unaosababishwa na risasi, taka, na maji taka yasiyotibiwa umefanya uzalishaji wa chakula kuwa jambo lisilowezekana,” alieleza Emine Erdogan kwa masikitiko.

“Wakati Israel inatekeleza mauaji ya halaiki mabaya zaidi katika historia huko Gaza, pia imesababisha uharibifu mkubwa wa mazingira na ikolojia ya eneo hilo,” alisema.

Aliongeza ya kuwa: “Kutokana na uharibifu huo huko Gaza, tani milioni 61 za vifusi zimebakia, ambazo huenda zikachukua karne nzima kuzisafisha. Asilimia 97 ya mazao ya miti, asilimia 82 ya mazao ya kila mwaka, na asilimia 95 ya maeneo ya vichaka yameharibiwa.”

Akizungumzia hali ya Gaza, alisema: “Hakuna mahali tena pa watu kuishi, hakuna ardhi ya kulisha mifugo, wala mazingira kwa ndege na viumbe kuendelea kuishi. Hivyo basi, tukazie jambo hili: Ikiwa vita vitaendelea, hatuwezi kutibu majeraha ya mazingira asili.”

CHANZO:TRT World