UTURUKI
2 dk kusoma
Uturuki kuendelea kuiunga mkono Gaza na kuleta matumaini kwa Wapalestina: Fidan
“Uturuki itaendelea kuwa pumzi kwa Gaza na matumaini kwa Palestina. Pia tutaendelea kuunga mkono kwa vitendo juhudi za kuijenga upya Gaza,” Hakan Fidan amesema.
Uturuki kuendelea kuiunga mkono Gaza na kuleta matumaini kwa Wapalestina: Fidan
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki asema kutekelezwa kwa suluhisho la mataifa mawili ni hatua ya kimsingi kuelekea amani ya kudumu katika eneo hilo. / / AA
tokea masaa 10

"Uturuki itaendelea kuwa pumzi kwa Gaza na matumaini kwa Palestina. Pia tutaendelea kuunga mkono kikamilifu juhudi za kuijenga upya Gaza," Fidan alisema Ijumaa katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na mwenzake wa Ujerumani Johann Wadephul.

“Kila jengo litakalojengwa Gaza litakuwa ni kazi ya dhamira ya pamoja ya ubinadamu. Lengo letu kuu ni kutekeleza suluhisho la mataifa mawili na kuanzisha Mashariki ya Kati yenye amani na ustawi licha ya mateso yote.”

Alisema kuwa Ankara iliongeza juhudi za misaada mara tu baada ya usitishaji mapigano kuanza, akisisitiza kuwa msaada wa kibinadamu kwa Gaza unapaswa kuwa wa muda mrefu na wa mfumo wa kudumu.

Katika mazungumzo yake na Wadephul, Fidan alisema ya kuwa Ankara na Berlin walikubaliana kuhusu umuhimu wa kuendelea kwa usitishaji mapigano Gaza, misaada ya kibinadamu kuwafikia wahitaji bila vikwazo, na kuhakikisha kuwa vita vinamalizika kabisa.

Kikosi kazi, baraza la amani

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki alisisitiza kuwa kutekeleza suluhisho la mataifa mawili ni hatua ya msingi kuelekea amani ya kudumu katika ukanda huo.

Aidha, alisisitiza umuhimu wa mataifa ya Ulaya – hususan Ujerumani – kuchukua hatua za kujenga ili kushughulikia masuala ya Palestina na Gaza.

Fidan alisema: “Uturuki imetekeleza majukumu yake katika utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa, na iko tayari kikamilifu kufanya zaidi kwa siku zijazo.”

Aliongeza kuwa katika mfumo huo, kuna dhamira ya dhati kutoka kwa Rais wa Uturuki kushiriki katika utekelezaji wa masuala kama vile “kikosi kazi, baraza la amani, au kikosi cha kimataifa cha kuleta utulivu,” pale vitakapoanza kutekelezwa.

CHANZO:TRT World