Mke wa Rais wa Uturuki Emine Erdogan ameadhimisha miaka miwili ya mauaji ya halaiki ya Israel huko Gaza, akishtumu Israel kwa kujaribu kuangamiza watu wa Palestina huku dunia ikiangalia.
“Taifa ambalo limepoteza dira yake ya maadili linataka kuangamiza watu wa Palestina huku dunia ikiangalia,” amesema Erdogan katika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa Uturuki NSosyal.
“Na huku unyama wa wanaodhulumu ukiongezeka, na ndivyo sauti za mioyo ya watu iliyoungana zinavyopazwa dhidi ya mauaji ya halaiki,” aliongeza.
Erdogan amesema kuwa katika kipindi cha miaka miwili, Gaza imekuwa sehemu ya makaburi ambapo watu zaidi ya 67,000 wasio na hatia, ikiwemo watoto zaidi ya 20,000, wameuawa, na utu wa ubinadamu umezikwa ukiwa hai.
Alisisitiza kuwa mashambulizi ya Israel, “hakuna mipaka yoyote si ya heshima, sheria, haki za binadamu, au maadili ambayo haijakiukwa.”
Amesema watu wamejitolea kusaidia Gaza kutoka kila pembe ya dunia, kwa ndege, njia za ardhini, na kwa bahari, pengine akiashiria kuhusu msafara wa meli za misaada za hivi karibuni katika bahari ya mediterani kuelekea eneo hilo ambalo limezingirwa, na kutoa wito “kwa kila mtu aliyeguswa na hili kuungana kwenye harakati hizi kwa pamoja kwa ajili ya Palestina hadi pale amani ya haki na ya kudumu itakapopatikana.”
“Naadhimisha kuwatakia rehma ndugu zetu wa Palestina waliokufa mashahidi kutokana na mashambulizi ya Israel, na naomba Allah Mtukufu kuwafanyia wepesi na kuwapa ushindi watu wa Palestina majasiri ambao, kwa subira yao, wanaendelea kuwa imara. #EndlessGenocideGaza,” alisema.
Ujumbe huo pia ulijumuisha video zilizoonesha hotuba za zamani za Erdogan kuhusu Gaza pamoja na video zilizoonesha namna gani hali ilivyo mbaya katika kanda hiyo.