| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Tanzania yatoa msaada wa chakula Msumbiji kufuatia mafuriko ya nchi hiyo
Shehena hiyo ya msaada ilifika jijini Maputo na ndege ya mizigo ya Shirika la Ndege la Tanzania.
Tanzania yatoa msaada wa chakula Msumbiji kufuatia mafuriko ya nchi hiyo
Tanzania na Msumbiji zimekuwa na ushirikiano wa muda mrefu. Picha/ Ofisi ya Waziri Salim Cripton Valá / TRT Afrika Swahili
tokea masaa 3

Tanzania imeikabidhi Msumbiji msaada wa mahindi tani 500 kufuatia mafuriko yaliyoikumba nchi hiyo kutokana na mvua kubwa zilizonyesha.

Msaada huo umekabidhiwa Machi 24, 2026.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Mahmoud Thabit Kombo, aliukabidhi msaada huo Machi 24, 2026 kwa Ujumbe wa Serikali ya Msumbiji uliongozwa na Waziri wa Mipango na Maendeleo Salim Cripton Valá.

"Kwa niaba ya Serikali ya Tanzania, Rais Samia anatoa salamu za pole kwa Rais wa Msumbiji, Mhe. Daniel Chapo na watu wa Msumbiji kwa ujumla kutokana na madhila yaliyosababishwa na mafuriko haya na ameahidi kuwa Tanzania ipo tayari kundelea kutoa msaada kwa Msumbiji katika nyakati zote," alisema Waziri Kombo wakati wa makabidhiano.

Shehena hiyo ya msaada ilifika jijini Maputo na ndege ya mizigo ya Shirika la Ndege la Tanzania.

Tanzania na Msumbiji zimekuwa na uhusiano wa karibu wa muda mrefu. Kwa mujibu wa Waziri Kombo, msaada huo ni muendelezo wa udugu uliopo kati ya mataifa hayo mawili.

Kwa upande wake, Msumbiji imeishukuru Tanzania.