UTURUKI
2 dk kusoma
Uturuki inaonya raia wanaojitolea kwa jeshi la Israel wanaweza kupoteza uraia
Naibu mwenyekiti wa chama tawala cha Uturuki cha AK anasema kuhudumu katika jeshi la kigeni bila kibali cha serikali ni sababu za kunyimwa uraia chini ya sheria za Uturuki.
Uturuki inaonya raia wanaojitolea kwa jeshi la Israel wanaweza kupoteza uraia
Takwimu za Wizara ya Mambo ya Ndani zinaonyesha kuwa raia wa Kiyahudi 29,178 wanaishi Uturuki, kati yao 1,568 pia wana uraia wa Israel. / / AP
tokea masaa 13

Uturuki imetoa onyo la wazi kwa raia wake kufuatia ripoti kuwa baadhi ya watu wamejitolea kuhudumu katika jeshi la Israel.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Ankara siku ya Ijumaa, Ozlem Zengin, naibu mwenyekiti wa chama tawala cha Haki na Maendeleo (AK Party), aliashiria kuwa sheria ya Uturuki inakataza waziwazi raia kujiunga na majeshi ya kigeni bila idhini rasmi ya serikali.

"Huduma ya kujitolea katika jeshi la kigeni bila idhini ya Jamhuri ya Uturuki ni sababu za kupoteza uraia," Zengin alisema, akinukuu vifungu vya sheria ya utaifa.

Aliwasilisha kusema ya kwamba takwimu za Wizara ya Mambo ya Ndani zinazoonyesha kuwa raia wa Kiyahudi 29,178 wanaishi Uturuki, kati yao 1,568 pia wana uraia wa Israel. Hawa ni pamoja na raia 426 wa Uturuki wenye uraia wa Israel na raia 1,142 wa Israel ambao baadaye walipata uraia wa Uturuki, wakijumuisha wanaume, wanawake na watoto.

Uchunguzi kuendelea

Kufikia sasa, ni mtu mmoja tu ambaye ameshitakiwa na kesi hiyo nchini Uturuki kwa kujitolea kwa huduma ya hiari katika jeshi la Israel, wakati kesi zingine mbili zinaendelea kuchunguzwa, Zengin alibainisha.

"Kubatilisha uraia kunawezekana chini ya sheria ya sasa, lakini lazima kuwepo kwa ushahidi na uthibitisho rasmi," alithibitisha.

Zengin pia alisisitiza kuwa Israel inatumia sera sawa ya visa kwa raia wa Kiyahudi kutoka Uturuki kama inavyofanya kwa raia wengine wa Uturuki, akisisitiza, "Hakuna msamaha unaotegemea dini au asili ya kabila."

CHANZO:TRT World