Raia wa Côte d'Ivoire wanapiga kura ya urais Jumamosi huku kiongozi aliye madarakani kwa sasa Alassane Ouattara, 83, akitafuta kurudi kwa muhula wa nne. Kuna wagombea wengine wanne wanaokabiliana naye kwenye uchaguzi.
Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Fedha la IMF, Ouattara aliingia madarakani 2011 badaa ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miezi minne vilivyosababisha vifo vya watu karibu 3,000. Anasisitiza kuwa ukuaji wa uchumi na usalama katika kipindi cha miaka 15 yeye ndiye aliyefanikisha hilo.
Vita vilisababishwa na mtangulizi wake, Laurent Gbagbo, kukataa kushindwa kwenye uchaguzi wa 2010.
Côte d'Ivoire, nchi inayozalisha kakao kwa wingi kote duniani, ni moja ambayo uchumi wake unakuwa kwa kasi Afrika Magharibi na dhamana zake ni moja kati ya bora barani Afrika.
Mshindi anapatikana vipi
Wanasiasa kadhaa mashuhuri wamezuiwa kushiriki katika uchaguzi huu, kufanya upinzani kuwa mdogo dhidi ya Ouattara.
Mmoja wao, Tidjane Thiam wa chama cha PDCI hakuruhusiwa kwenye daftari wapiga kura kutokana na uraia pacha wa Ivory Coast na Ufaransa. Aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Laurent Gbagbo wa chama cha PPA-CI pia hakuruhusiwa.
Vyama vyao havijawasilisha majina ya wagombea mbadala. Jean-Louis Billon, mwenye umri wa 61, ambaye aliondoka kwenye chama cha PDCI cha Tidjane Thiam, sasa anawania kwa tiketi ya chama cha Democratic Congress
(CODE).
Wengi wanamuona mke wa rais wa zamani Simone Éhivet Gbagbo mwenye umri wa miaka 76, kama mgombea wa ajabu kwenye uchaguzi huu. Alijitokeza kama mgombea wa chama cha Movement of Capable Generations (MGC) baada ya aliyekuwa mume wake Laurent Gbagbo kuzuiwa kugombea.














