AFRIKA
1 dk kusoma
Mfalme Mohammed VI anatarajiwa kutoa hotuba huku vijana (Gen Z) wakitaka mabadiliko Morocco
Mfalme wa Morocco Mohammed VI anafungua bunge siku ya Ijumaa kwa hotuba, huku maandamano yakirindima dhidi ya serikali kote nchini.
Mfalme Mohammed VI anatarajiwa kutoa hotuba huku vijana (Gen Z) wakitaka mabadiliko Morocco
Waandamanaji nchini Morocco. / Reuters
tokea masaa 16

Tangu Septemba 27, waandamanaji wamekuwepo barabarani katika miji kadhaa nchini Morocco, wakipinga matumizi ya mabilioni ya fedha yanayoelekezwa katika maandalizi ya Kombe la Dunia 2030.

Vijana hao wanaojiita wanaharakati wa “Gen Z 212” wamekuwa wakiandamana katika maeneo ya viwanja vipya wakidai kutelekezwa kwa huduma za msingi za umma. Vijana hao wamehamasishana kupitia mitandao ya kijamii kama TikTok na mingineyo.

Hotuba hii inakuja wiki moja baada ya maandamano ya vijana ambao walituma barua moja kwa moja katika kasri la mfalme wakieleza malalamiko yao.

Walitaka kufutwa kazi kwa Waziri Mkuu Aziz Akhannouch na serikali yake, kuachiliwa huru kwa wafungwa wa kisiasa, na kuundwa kwa jukwaa litakalo wawajibisha wanasiasa mafisadi.

CHANZO:TRT Afrika Swahili