Kuanzia Oktoba 23, nchi hiyo ya Afrika Mashariki itakuwa katika kundi la nchi saba za Afrika, ambazo raia wake watatakiwa kulipa dhamana itakayorudishwa ya kati ya dola 5,000, sawa na shilingi milioni 12 za Tanzania au dola 15,000 ambazo ni sawa na shilingi milioni 37.
Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, agizo hilo linawahusu wale watakaoomba viza kwa ajili ya biashara B-1 (Business) na utalii B-2 (Tourism).
Serikali ya Marekani imesema agizo hilo linafuatia taarifa za baadhi ya raia kutoka mataifa hayo kupitiliza muda wao pindi wanapokuwa nchini Marekani.
Hata hivyo, serikali ya Tanzania, imesema tayari imeingia katika mazungumzo na Marekani kuona ni jinsi gani nchi mbili hizo zinaweza kufikia muafaka wa kukabiliana na changamoto hiyo.
Miongoni mwa nchi hizo ni pamoja na Mali na Mauritania, agizo hilo litaanza rasmi Oktoba 23, 2025.