AFRIKA
1 dk kusoma
Tshisekedi wa DRC amtaka Kagame wa Rwanda 'kukumbatia amani' katika mkutano jijini Brussels
Rais Felix Tshisekedi ametoa wito kwa mwenzake wa Rwanda Paul Kagame "kukumbatia amani" na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Tshisekedi wa DRC amtaka Kagame wa Rwanda 'kukumbatia amani' katika mkutano jijini Brussels
Rais Felix Tshisekedi ametoa wito kwa mwenzake wa Rwanda, Paul Kagame, kukumbatia amani mashariki mwa DRC. / Picha: AA
tokea masaa 17

Rais Felix Tshisekedi ametoa wito kwa mwenzake wa Rwanda Paul Kagame "kukumbatia amani" na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Tshisekedi, 62, alitoa wito huo katika mkutano jijini Brussels, Ubelgiji baada ya Kagame kuhutubia kongamano hilo.

"Natoa wito na mkutano huu ni mashahidi, na dunia nzima, kutafuta amani, Bwana Rais, ili tuweze kuwa na amani," Tshisekedi alisema.

Mashariki mwa DRC, eneo linalopakana na Rwanda na lina raslimali nyingi za asili, limekumbwa na vurugu kwa zaidi ya miongo mitatu. DRC inadai Rwanda inaunga mkono kundi la waasi la M23, ambalo linaendeleza harakati zake mashariki mwa DRC, lakini Rwanda inakanusha.

M23 imedhibiti maeneo mengi mashariki mwa DRC

Kundi la waasi wa M23, ambalo lilianza tena mapigano mwishoni mwa mwaka 2021, limedhibiti maeneo mengi katika kanda hiyo, na kusababisha matatizo makubwa kwa watu.

Kagame, ambaye alikuwepo kwenye kongamano hilo la Brussels, hakuzungumzia mzozo huo moja kwa moja katika hotuba yake, ingawa aligusia kuhusu hotuba ya awali ya Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, ambaye alisema anahisi "kuna uwezekano wa kupatikana kwa amani" alipowaona viongozi wa Rwanda na DRC.

"Baadhi yetu pia tumehisi hivyo hivyo. Tumehisi uwezekano huo kuhusu biashara zetu, uwekezaji, amani," Kagame alisema.

CHANZO:TRT Afrika Swahili