ULIMWENGU
1 dk kusoma
FIFA haiwezi kutatua ‘masuala ya siasa za nchi’, asema Infantino
Mwaka 2022, FIFA iliifungua Urusi baada ya majeshi yake kuivamia Ukraine, licha ya Urusi kuandaa fainali ya Kombe la Dunia, hapo awali.
FIFA haiwezi kutatua ‘masuala ya siasa za nchi’, asema Infantino
Rais wa FIFA Gianni Infantino./Picha:Wengine
2 Oktoba 2025

Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) Gianni Infantino amesema kuwa taasisi hiyo haiwezi kutatua ‘siasa za nchi’, licha ya kuendelea kupata shinikizo la kuisimamisha uanachama Israel kufuatia mashambulizi yake dhidi ya Palestina.

Kupitia taarifa yake, Infantino "aligusia umuhimu wa kuimarisha amani na umoja kwenye muktadha wa kinachoendelea Gaza.”

"Kama FIFA, tunatumia mchezo wa soka kuwaleta watu pamoja," alisema Infantino.

"Fikra zetu zipo kwa wale wanaoendelea kuteseka maeneo mbalimbali yaliyokumbwa na machafukio, ila kwa sasa ujumbe mahususi kwa sasa ni umoja na amani."

"FIFA haiwezi kutatua masuala ya nchi, lakini ina wajibu wa kukuza mchezo wa soka ulimwenguni, kwa kufanya nyenzo ya kuunganisha watu," aliongeza.

Mwaka 2022, FIFA iliifungua Urusi baada ya majeshi yake kuivamia Ukraine, licha ya Urusi kuandaa fainali ya Kombe la Dunia, hapo awali.

CHANZO:AFP