ULIMWENGU
1 dk kusoma
Marekani yapongeza azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu usalama wa Haiti
Uamuzi huo unakuja baada ya baraza hilo kuidhinisha kikosi kipya cha kulinda usalama nchini Haiti.
Marekani yapongeza azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu usalama wa Haiti
Wajumbe wa Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa./Picha:@UN_News_Centre
1 Oktoba 2025

Marekani imepongeza azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuidhinisha kikosi kipya cha kulinda usalama nchini Haiti, kijulikanacho kama ‘Gang Suppression Force (GSF)’.

Kikosi hicho, ambacho kitahudumu kwa miezi 12, kinachukua nafasi ya ‘Multinational Security Support (MSS)’, ambacho pia kilihusisha askari kutoka Kenya.

“Marekani itaendelea kufanya kazi na wadau mbalimbali kuisaidia Haiti iweze kupata amani na utulivu,” alisema Marco Rubio, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani.

Aliongeza: Ujumbe kutoka baraza hilo ni wazi kabisa: Wale wenye nia ya kuendeleza vurugu nchini Haiti, siku zao zimekwisha.

Azimio hilo, ambalo limefadhiliwa kwa pamoja na Panama na Marekani, pia limeidhinisha kuanzishwa kwa ofisi maalumu ya Uratibu ya Umoja wa Mataifa (UNSOH).

Wakati huo huo, Rubio aliopongeza Kenya na mataifa mengine yaliyochangia kwenye operesheni maalumu ya ulinzi wa amani Haiti, ambayo ilianza Juni 2024, ikifikia tamati Oktoba 2.

Zaidi ya watu milioni 1.3 wamekimbia makazi yao nchini Haiti kutokana na vurugu, idadi kubwa zaidi katika historia ya nchi hiyo na karibu nusu ya nchi inakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula.

 

CHANZO:AA