6 Oktoba 2025
Rais wa Madagascar Andry Rajoelina amemteua Ruphin Fortunat Zafisambo, jenerali wa jeshi, kuwa waziri mkuu mpya wa nchi siku ya jumatatu, wiki moja baada ya kuvunja baraza la mawaziri.
"Kwa hekima kabisa, nimeamua kumteua Ruphin Fortunat Dimbisoa Zafisambo, Jenerali, kuwa Waziri Mkuu wa serikali," kiongozi wa nchi amesema.
Hili linatokea wakati maandamano yakiingia wiki yake ya tatu siku ya Jumatatu.
Maandamano, yalichochewa na raia kuteta kuhusu kukatika kwa umeme na uhaba wa maji, ambayo yameendelea na kuonesha ishara ya kutokuwa na imani na serikali ya sasa.
Hata hivyo, Rais Rajoelina, 51, anasema kuwa "ni njama za wanasiasa" wenye lengo la "kutatiza" Madagascar.
CHANZO:TRT Afrika Swahili