Kitengo cha Mifugo na Ukamataji wa Huduma ya Wanyamapori Kenya, KWS kilifanikiwa kumhamisha tembo dume kutoka na usumbufu wake, kutoka Kijiji cha Kithoka karibu na Msitu wa Imenti, Kaunti ya Meru, hadi Mbuga ya Kitaifa ya Tsavo Mashariki zaidi ya kilomita 400.
Tembo huyo alikuwa anafahamika wa kuvunja uzio wa umeme na kuvamia mimea, na hivyo kusababisha tishio kwa maisha ya wenyeji.
“Uhamisho huu ulimzuia fahali kufundisha wengine mbinu zake za kuvunja uzio na kumhakikishia ustawi katika eneo kubwa la kilomita za mraba 13,700 la Tsavo Mashariki.”
KWS inasema kuwa ili kupunguza mzozo kati ya wanyama na wanadamu jitihada kama hizi ni lazima zifanyike.
“Ili kupunguza migogoro hiyo, KWS inaendelea kutekeleza hatua kama vile uzio wa kimkakati na, inapobidi, kuhamisha wanyama wenye matatizo.”