AFRIKA
1 dk kusoma
Watu wasiopungua 13 wauawa, 19 wajeruhiwa katika mashambulizi ya makombora ya RSF huko Darfur Sudan
Raia wasiopungua 13 wameuawa na wengine 19 kujeruhiwa katika mashambulizi ya makombora ya wapiganaji wa RSF Kaskazini mwa Darfur, madaktari wa eneo hilo wamesema siku ya Jumatatu.
Watu wasiopungua 13 wauawa, 19 wajeruhiwa katika mashambulizi ya makombora ya RSF huko Darfur Sudan
Watu wasiopungua 20,000 wameuawa kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe Sudan tangu vilipoanza katikati ya mwezi April 2023./ Picha: AP
6 Oktoba 2025

Raia wasiopungua 13 wameuawa na wengine 19 kujeruhiwa katika mashambulizi ya makombora ya wapiganaji wa RSF Kaskazini mwa Darfur, madaktari wa eneo hilo wamesema siku ya Jumatatu.

Mtandao wa Madaktari wa Sudan unasema watu waliojeruhiwa wanajumuisha watoto saba na mwanamke mmoja mjamzito katika shambulio lililolenga eneo la makazi huko El-Fasher, mji kuu wa Kaskazini mwa Darfur magharibi mwa Sudan.

Kundi hilo la madaktari linasema raia kadhaa walikuwa bado wamekwama huku eneo hilo likishambuliwa.

lilishtumu mashambulizi hayo ya RSF kama “uhalifu kamili na kulenga kwa maksudi maisha ya raia,huku jamii ya kimataifa ikiwa imenyamaza kimya bila kuona aibu na kushindwa kulinda maisha ya maelfu ya wakazi waliokwama kwenye mji huo.”

Wito wa hatua za haraka

Kundi hilo limetoa wito kwa jamii ya kimataifa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuchukuwa hatua za haraka kuzuia mashambulizi dhidi ya raia na kuhakikisha raia wanalindwa pamoja na wafanyakazi wa afya.

RSF imeweka vizuizi El-Fasher tangu Mei 10, 2024, licha ya onyo la kimataifa kuhusu hatari kwa mji huo, ambapo shughuli za kutoa misaada kwa majimbo yote matano ya Darfur zimekuwa zikifanyika.

CHANZO:AA