tokea saa limoja
Mahakama moja jijini Moscow imeitoza faini ya Dola 139,000 kampuni ya teknojolia ya Google kwa kukataa kuondoa taarifa iliyopigwa marufuku nchini Urusi.
Kulingana na taarifa iliyotolewa na Mahakama ya Wilaya ya Tagansky, kampuni ya Google ilikiuka sheria za nchi hiyo kwa kushindwa kuzuia usambazwaji wa taarifa ambazo zilipigwa marufuku nchini Urusi.
"Mahakama imeikuta Google na hatia chini ya kifungu cha sheria zenye kudhibiti usambazaji wa taarifa," ilisomeka sehemu ya taarifa ya mahakama hiyo.
Kuanzia mwaka 20189, mitandao mbalimbali ya nchini Marekani ikiwemo X, Facebook, Instagram na LinkedIn na YouTube, ilipigwa marufuku nchini Urusi kwa kushindwa kufuata sheria za nchi hiyo.
CHANZO:AA








