tokea masaa 13
Urusi na Ethiopia, zilisaini mpango wa kuanzisha mradi wa kiwanda cha nishati siku ya Alhamisi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Rosatom, Alexey Likhachev, na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia, Gedion Timotheos, walisaini mkataba huo jijini Moscow mbele ya Rais wa Urusi, Vladimir Putin, na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed.
Pande zote mbili pia zilisisitiza ushirikiano katika sekta za nishati na miundombinu.
Zilizopendekezwa
Rosatom ni shirika la serikali la Urusi linalohusika na nishati ya atomiki, lililoanzishwa mwaka 2007.
Nchi hizo mbili zilisaini makubaliano kuhusu ushirikiano katika matumizi ya amani ya nishati ya nyuklia mwaka 2017, ambayo yaliweka msingi wa ushirikiano mpana zaidi katika sayansi ya nyuklia, teknolojia na elimu.