Utajiri wa Afrika: Michoro ya miamba ya Malawi
Utajiri wa Afrika: Michoro ya miamba ya Malawi
Wataalamu wanasema michoro mingi ilitengezwa katika kipindi cha zaidi ya miaka 1,000 iliyopita, kufuatia kuhama kwa wakulima wa Chewa katika eneo hilo.
tokea masaa 8

Katika milima yenye miti kaskazini-magharibi mwa Dedza, Malawi ya Kati, kuna eneo lenye Sanaa ya Miamba linaloitwa Chongoni.

Hapa kuna maeneo 127 yenye majiwe makubwa na urembo wake ni michoro kwenye mawe haya.

Zinajumuisha nguzo nene zaidi za sanaa ya miamba inayopatikana Afrika ya kati.

Wataalamu wanasema michoro mingi ilifanywa katika kipindi cha zaidi ya miaka 1,000 iliyopita, kufuatia kuhama kwa wakulima wa Chewa katika eneo hilo.

Walianzisha uchoraji na udongo mweupe, ambapo wenyeji wa awali, wawindaji wa Batwa, walikuwa na utamaduni wa kuchora rangi nyekundu.

Picha zao zinahusishwa haswa na unyago, utayarishaji wa mvua na ibada za mazishi ya wanawake, mila ambazo zinaendelea katika jamii ya Wachewa hadi leo kwa wanaoishi katika maeneo hiyo.

Wamalawi wanathamini michoro hii kama utamaduni wa sanaa ya miamba ya wakulima, ambayo ni nadra.

Michoro hii inahusishwa sana na wanawake na bado ina umuhimu wa kitamaduni hadi leo katika kabila la Wachewa.

Eneo hilo sasa ni Tovuti ya Urithi wa Dunia wa UNESCO.

Sanaa ya miamba inaendelea katika hali yake ya awali mbali na michakato ya hali ya hewa ya asili kwa muda, matatizo fulani na uharibifu wa maji.

Uadilifu wa michoro ya miamba katika mazingira yao ya asili umeathiriwa kwa kiwango kidogo.

Watu waliokuwa wakiishi katika eneo hilo walihamishwa wakati msitu huo ulipotangazwa kuwa hifadhi.

Changamoto nyingine pia ni ukosefu wa wafanyakazi wa kudumisha uasili wa miamba hii ya chongoni.

Hata hivyo urembo wa michoro ya Chongoni unabaki kuwa kivutio cha kipekee kwa yeyeote anayeitembelea Malawi.