"Tumeshachukua mamlaka," alisema Kanali Michael Randrianirina, ambaye aliongoza uasi wa wanajeshi waliojiunga na waandamanaji wa kizazi cha Gen Z wanaopinga serikali, alipokuwa akizungumza kupitia redio ya taifa.
Randrianirina aliongeza kuwa jeshi linavunja taasisi zote za serikali isipokuwa Bunge la Chini (Baraza la Wawakilishi), ambalo lilikuwa limepiga kura ya kumng’oa madarakani Rajoelina dakika chache kabla ya tangazo hilo.
Katika siku ya machafuko kwa taifa hilo nje ya Afrika mashariki, kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 51 alitoa amri ya kuvunja bei kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook.
Licha ya kusafiri kwa ndege ya kijeshi ya Ufaransa, Rajoelina anakataa kuachia ngazi baada ya wiki kadhaa za maandamano ya waandamanaji wa kizazi cha Gen Z wanaomtaka ajiuzulu, pamoja na kuwepo kwa uasi wa kijeshi.
Ofisi ya rais haikujibu mara moja hatua ya Randrianirina lakini awali ilisema mkutano wa bunge ulikuwa kinyume cha katiba na hivyo hatua yoyote ni "batili."
Rajoelina amesema amehamia sehemu salama kwa sababu ya vitisho vya maisha yake. Afisa wa upinzani, chanzo cha kijeshi na mwanadiplomasia wa kigeni aliiambia shirika la habari la Reuters kuwa alitoroka nchini Jumapili kwa ndege ya kijeshi ya Ufaransa.