16 Septemba 2025
Simba Sports Club imeendeleza ‘uteja’ wake mbele ya mahasimu wao Young Africans, baada ya kufungwa bao 1-0, katika mchezo wa Ngao ya Jamii, uliofanyika Septemba 16, 2025, katika uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.
Bao pekee la ‘Wananchi’ lilipatikana katika dakika 53 ya mchezo, kupitia kwa mchezaji wao nyota, Pacome Zouzoua, na hivyo kuifanya Simba kupoteza mchezo wao wa sita mfululizo katika michezo tofauti, mbele ya mahasimu wao wa jadi.
Zilizopendekezwa
CHANZO:TRT Afrika Swahili