Bunge limeibua wasiwasi juu ya gharama za ukarabati wa magari zinazofanywa na Mamlaka ya Mapato ya Uganda (URA) baada ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kufichua kuwa katika kipindi cha miaka mitatu, Mamlaka hiyo ilitumia zaidi ya dola milioni 1.84( UGshs 6.4 bilioni ) kukarabati magari 61, huku kila gari likigharimu wastani wa zaidi ya dola 21,900 ( Ugshs milioni 77).
Gharama kubwa iliyotumika kukarabati gari ikiwa ni zaidi ya dola 30,000 (UGShs106 milioni).
Ufichuzi huo ulitolewa na Medard Sseggona mbunge wa Busiro Mashariki wakati akiwasilisha ripoti ya Kamati ya Tume, Mamlaka za Kisheria na Biashara za Serikali (COSASE) kuhusu ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Mamlaka ya Mapato ya Uganda - Huduma za Biashara ya Disemba 2024, wakati wa kikao cha mawasilisho cha Septemba 11, 2025.
“Gharama hii kubwa katika ukarabati wa magari ni kiashiria cha magari ya zamani yasiyo na thamani kiuchumi,” Sseggona alisema.
Uongozi wa URA ulieleza kuwa magari yametumika kwa wastani wa miaka 8-12 na kufanyiwa matengenezo makubwa na kati ya magari 6l yaliyochaguliwa, magari 12 yamefanyiwa ukarabati wa injini, 21 yalipelekwa mikoani na 16 yalikuwa katika oparesheni za kiuslama
URA imeliarifu bunge kuwa rasilimali za kununua magari mapya zilitolewa kwa mwaka wa fedha 2024/25 kwa zaidi ya dola milioni 1.9 na kwamba mchakato wa ununuzi wa magari 25 ya ziada umeshaanzishwa na upo kwenye hatua za ukandarasi, unasubiri kibali cha Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Magari mengine 25 yanatarajiwa kufikia Disemba 2025, ilhali kuondolowa kwa magari makuu 38 inatimizwa.
Hata hivyo, Kamati ilionyesha wasiwasi wa ucheleweshwaji wa utoaji wa magari hayo, ikitolea mfano mwaka wa fedha wa 2021/22 ambapo URA ilinunua magari 132 kuchukua nafasi ya yaliyozeeka lakini haya yalichukua muda mrefu kufikishwa.
Mbunge huyo Ssegona huyo amelalamika kuwa muda iliyochukua muuzaji kuleta magari hayo ni mrefu mno na hivyo kuathiri shughuli hiyo.
Bunge lilipitisha mapendekezo ya Kamati inayomtaka Kamishna Jenerali ya URA kuhakikisha ununuzi na uwasilishaji wa haraka wa magari mapya, pamoja na kuharakisha uondoaji wa magari chakavu, ili kupunguza gharama za matengenezo ya gari.