Afrika Kusini yaanzisha mwalimu wa roboti wa AI
AFRIKA
1 dk kusoma
Afrika Kusini yaanzisha mwalimu wa roboti wa AIRoboti huyo anayejulikana kama IRIS, ana uwezo kufunza kwa kutumia lugha za Afrika Kusini, ikiwemo isiZulu, Afrikaans, Sesotho, na Kiingereza.
Roboti IRIS wa Afrika Kusini.
tokea masaa 11

Afrika Kusini imeanzisha enzi mpya katika masuala ya elimu kwa kuzindua roboti wa Akili Mnemba anayefunza. Ni teknolojia ya kwanza barani Afrika.

Maafisa wameuita ubunifu huu wenye lengo la kuimarisha mafunzo madarasani.

Roboti IRIS aliundwa na shirika la BSG Technologies, kampuni ya masuala ya teknolojia ya Afrika Kusini.

Roboti anazungumza lugha mbalimbali, na ana uwezo wa kufunza masomo yote kuanzia shule za chekechea hadi chuo kikuu. Anawasiliana kwa lugha zote rasmi za Afrika Kusini, ikiwemo isiZulu, Afrikaans, Sesotho, na Kiingereza.

Muasisi wa kampuni hiyo ni raia wa Afrika Kusini Thandoh Gumede, mwenye umri wa miaka 31, na mwalimu wa zamani katika eneo la vijijini la Hluhluwe mkoa wa KwaZulu Natal. Gumede anasema alianza kufanyia kazi mradi huo miaka minane iliyopita.

Mwalimu roboti anajibu anaposikia sauti, na kufanya mazingira ya masomo kuwa ya kuwasiliana na kuhamasisha wanafunzi, hasa katika maeneo ya vijijini.

Gumede ameweka lengo la kumfikisha roboti katika kila darasa Afrika Kusini, lakini amesisitiza kuwa itabidi washirikiane na wadau wengine katika maendeleo ili hilo litimie.

Wakati wa uzinduzi mjini Durban mwezi Agosti, Naibu Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu, Nomalungelo Gina, ameutaja ubunifu huo kama hatua muhimu ambayo “itawawezesha wanafunzi kutimiza malengo ya kupata mafunzo.”

CHANZO:TRT Afrika