| swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Jeshi la Madagascar laweka pembeni katiba, latangaza kipindi cha mpito cha miaka miwili
Kikosi maalum cha kijeshi cha CAPSAT, kilitangaza Jumanne kusimamisha utekelezwaji wa Katiba na kuchukua mamlaka baada ya Bunge kumuondoa madarakani Rais Andry Rajoelina.
Jeshi la Madagascar laweka pembeni katiba, latangaza kipindi cha mpito cha miaka miwili
Jeshi la Madagascar limesema kipindi cha mpito kufuatia kuondolewa madarakani kwa Andry Rajoelina kitadumu kwa miaka miwili. /
14 Oktoba 2025

Kwa mujibu wa mwandishi wa shirika la habari la Anadolu, CAPSAT ilichukua hatua hiyo baada ya Bunge kupitisha azimio la kumuondoa madarakani Rais Rajoelina.

Kikosi cha CAPSAT, kikiongozwa na Kanali Michael Randrianirina, kiliingia katika Ikulu ya Ambohitsorohitra iliyoko katika mji mkuu, Antananarivo, na kutangaza kuchukua uongozi wa nchi.

Kanali Randrianirina alisema: "Kwa kutumia Amri namba 2025-001, tumeamua kusitisha utekelezwaji wa katiba iliyopitishwa Desemba 11, 2010, na kuanzisha mifumo mipya kwa ajili ya mageuzi ya kitaifa."

Aliongeza kuwa: "Kipindi cha mpito kitadumu kwa muda usiozidi miaka miwili. Katika kipindi hiki, kura ya maoni itafanyika ili kuunda katiba mpya, kisha uchaguzi utafanyika kuanzisha taasisi mpya hatua kwa hatua."

InayohusianaTRT Afrika - Jeshi lachukua nchi Madagascar

Taasisi zilizosimamishwa

 Taasisi tano zimesimamishwa kazi, nazo ni: Mahakama ya Katiba ya Juu, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Seneti, Baraza Kuu la Ulinzi wa Haki za Binadamu, na Mahakama ya Juu ya Haki.

Hata hivyo, Bunge la Taifa limesalia kama taasisi pekee inayofanya kazi.

Jeshi lilitangaza kuwa nafasi ya urais sasa itashikiliwa kwa pamoja na maafisa wake wa kijeshi.

Mapema siku hiyo, Rajoelina alivunja bunge kufuatia wiki kadhaa za maandamano dhidi ya serikali kote nchini, akisema ni muhimu kurejesha utulivu na kutoa nafasi kwa vijana. Hata hivyo, bunge lilipiga kura na kupitisha hoja ya kumuondoa rais mahakamani.

Rajoelina asema yuko "mahali salama" 

Tangu Septemba 25, Rajoelina amekuwa akikabiliwa na maandamano yanayoongozwa na vijana kutokana na ukosefu mkubwa wa maji na umeme, pamoja na tuhuma za ufisadi, ambayo baadaye yaligeuka kuwa wito wa kujiuzulu kwake.

Machafuko hayo yalisababisha mabadiliko makubwa serikalini, ikiwemo kuvunjwa kwa baraza la mawaziri na uteuzi wa waziri mkuu na viongozi wapya wa usalama.

Mnamo Jumatatu, Rajoelina alisema alikuwa amejificha "mahali salama" baada ya "jaribio la kumuua," huku ripoti zikidai kuwa alihamishiwa Ufaransa kwa ndege ya kijeshi baada ya kufikiwa kwa "makubaliano" na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.

Macron alikataa kuthibitisha iwapo Rajoelina alihamishiwa na Ufaransa, akisema akiwa nchini Misri kuwa: "Ninachoweza kusema ni kuwa tunatiwa wasiwasi sana na hali hiyo."

Rajoelina aitaja hali hiyo kuwa "jaribio la kupindua serikali kinyume cha sheria"

Mnamo Jumamosi, CAPSAT – kitengo cha kijeshi ambacho kilimsaidia Rajoelina kuingia madarakani kupitia mapinduzi mwaka 2009 – kilitangaza kuunga mkono maandamano ya wana Gen Z.

Jumapili, CAPSAT ilimteua mkuu mpya wa kijeshi, saa chache baada ya Rajoelina kulaani uungwaji wao mkono kwa maandamano hayo akisema ni "jaribio la kupindua serikali kinyume cha sheria."

InayohusianaTRT Afrika - Rais wa Madagascar avunja bunge huku mzozo wa kisiasa ukitikisa nchi

 

 

CHANZO:AA, TRT Afrika
Soma zaidi
Jaji Mkenya achaguliwa Mahakama ya Kimataifa ya Haki
Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini amfuta kazi makamu wake
Duma wa Botswana aipa India zawadi ya duma 8
Kesi ya Roger Lumbala wa DRC yaanza kusikilizwa
Kesi za ubakaji, watoto kupotea zaripotiwa Darfur, Sudan – Umoja wa Mataifa
Ugonjwa wa Kichaa cha mbwa barani Afrika: Janga linaloendelea kuathiri maisha japo linaepukika
Libya yatakiwa kufunga vituo vya kuwazuilia wahamiaji katika mkutano wa Umoja wa Mataifa
Rais Museveni aonya kuzuka kwa vita endapo nchi za Afrika zitashindwa kufikia Bahari ya Hindi
UN: Milioni 11 wanawake na wasichana wanabeba uzito mkubwa wakati njaa ya Sudan inaendelea kupamba moto
Ethiopia yachagguliwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya hewa, COP32
Ghana yafichua sababu ya ajali ya helikopta iliyoua watu wanane, wakiwemo mawaziri, mwezi Agosti
Nigeria yaanzisha uchunguzi baada ya kukamata kilo 1,000 za kokeini yenye thamani ya $235M
Kenya kuanzisha balozi zake mpya Vatican City, Denmark na Vietnam
Mtoto wa Gaddafi aachiliwa huru baada ya miaka kumi gerezani
Kuanzia vifo vya taratibu hadi mauaji ya ukatili: Kutoweka kwa utu Al Fasher
Zaidi ya mataifa 20 yanalaani ukatili wa RSF nchini Sudan, na kutaka kukomeshwa kwa ghasia
Rais wa Misri, afisa mkuu wa usalama wa Urusi kujadili ushirikiano wa kijeshi
Maelfu ya wananchi wanashikiliwa katika hali mbaya sana katika Al Fasher, Sudan: madaktari
Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance aghairi ziara iliyopangwa nchini Kenya
‘Mauaji ya waandamanaji ni chukizo mbele za Mungu’