tokea masaa 9
Timu hiyo ya Bafana bafana imefuzu Kombe la Dunia licha ya kuondolewa pointi tatu kwa kumchezesha mchezaji asiyestahili katika mechi za awali.
Hii itakuwa mara ya kwanza kwa Afrika Kusini kushiriki Kombe la Dunia tangu ilipofuzu moja kwa moja kama mwenyeji mwaka 2010.
Ushindi huo wa Afrika Kusini umeifanya Nigeria kumaliza katika nafasi ya pili kwenye kundi hilo, na sasa italazimika kushiriki hatua ya mchujo ili kufuzu.
Nigeria iliifunga Benin 4-0 nyumbani, baada ya mshambuliaji Victor Osimhen kufunga mabao matatu.
CHANZO:Reuters