Mwili wa kiongozi wa upinzani maarufu nchini Kenya, Raila Odinga, umewasili katika mji mkuu wa nchi hiyo Nairobi mapema Alhamisi kutoka India ambako alifariki dunia pindi alipokuwa akipata matibabu.
Umati mkubwa wa watu ulikusanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta ili kupokea jeneza lake, kwa mujibu wa AFP.
Rais William Ruto ametangaza siku saba za maombolezo ya kitaifa kwa heshima ya Odinga, ambaye aligombea urais mara tano bila mafanikio lakini alikuwa na nafasi kubwa katika siasa za Kenya kwa miongo kadhaa.
Mwili wa Odinga umepelekwa katika uwanja wa Kasarani ambapo viongozi pamoja na maelfu ya Wakenya kutoka maeneo mbalimbali watapata fursa ya kutoa heshima zao za mwisho.
Raila atazikwa siku ya Jumapili kando ya kaburi la mama yake huko Opodo, katika Kaunti ya Siaya.