Rais wa Ivory Coast, Alassane Ouattara, kwa mara nyingine ameshinda uchaguzi wa urais, kulingana na matokeo ya awali yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi siku ya Jumatatu.
Mwanasiasa huyo mwenye miaka 83, ambaye hapo awali alikuwa mfanyabiashara wa benki za kimataifa, alipata asilimia 89.77 ya kura.
Takriban raia milioni tisa wa Ivory Coast wamejisajili kupiga kura katika kinyang'anyiro ambacho kiliwatenga wapinzani wakuu wa Ouattara.
Jean-Louis Billon, waziri wa zamani wa biashara kutoka mojawapo ya familia tajiri zaidi za Ivory Coast, alishika namba mbili kwa kupata asilimia tatu 3 ya kura, kwa mujibu wa matokeo ya awali.
Simone Gbagbo, mke wa rais wa zamani wa Ivory Coast na mke wa Rais wa zamani Laurent Gbagbo, aliibuka wa tatu kwa kupata asilimia 2.4, chini ya matokeo ya utoaji.
Rais wa zamani Laurent Gbagbo alizuiliwa kushiriki uchaguzi huo kwa kosa la uhalifu, na Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa Credit Suisse Tidjane Thiam aliondolewa katika kinyang'anyiro hicho kwa kuchukua uraia wa Ufaransa.














