tokea masaa 11
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amemsimamisha Mkuu wa Idara ya Usalama nchini humo Imtiaz Fazel, kupisha uchunguzi kuhusiana na utendaji wake wa kazi.
Katika taarifa iliyotolewa Oktoba 15, kamati maalumu bunge la nchi hiyo, yenye kushughulikia masuala ya intelijensia , imesema kuwa ilimtaarifu Rais Ramaphosa kuwa ilipokea malalamiko juu ya mwenendo wa Fazel.
Hata hivyo, kamati hiyo haikuweza wazi makosa yanayomkabili mkuu huyo wa Idara ya Upelelezi nchini humo.
Kusimamishwa kwa Fazel kunakuja katikati ya sakata la tuhuma mbalimbali zinazolikabili jeshi la polisi la nchi hiyo pamoja na idara ya usalama hususani zile zinazomkabili kamishna wa Polisi katika eneo la KwaZulu-Natal, Nhlanhla Mkhwanazi mwezi Julai mwaka huu.
CHANZO:TRT Afrika Swahili