AFRIKA
2 dk kusoma
Umoja wa Afrika yamchagua Rais wa Uganda kuwa mpatanishi wa amani Sudan
Vita nchini Sudan vimekuwepo tangu Aprili 2023 na kusababisha maelfu kuhama makazi yao na wengine kukimbilia nchi za nje.
Umoja wa Afrika yamchagua Rais wa Uganda kuwa mpatanishi wa amani Sudan
Rais Yoweri Museveni ameteuliwa kuongoza mchakato wa amani nchini Sudan/ picha: Reuters
tokea masaa 8

Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika, limemuelekeza Mwenyekiti wa Tume ya AU ashirikiane kwa haraka na Wajumbe wa Kamati ya Madhubuti ya Rais ya PSC, chini ya uongozi wa Yoweri Kaguta Museveni, Rais wa Uganda, ili kuwezesha haraka mchakato wa mazungumzo kati ya viongozi wa Jeshi la Sudan (SAF) na wapiganaji wa kundi la Rapid Support Forces (RSF) ikiwa ni pamoja na kufanyika kwa Mkutano Maalum wa AU kuhusu Sudan.

“Kwa vitendo vya uhalifu dhidi ya raia wa Sudan na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na sheria za kimataifa, unaofanywa na RSF, baraza linatoa wito kwa kiongozi wa jeshi la RSF kuzingatia sheria ya kimataifa kwa haki za kibinadamu.” imesema katika taarifa.

Vita nchini Sudan vimekuwepo tangu Aprili 2023 na kusababisha maelfu kuhama makazi yao na wengine kukimbilia nchi za nje.

Baraza limetoa “ madai ya kusitishwa mara moja na bila masharti ya uhasama na kufunguliwa kwa njia salama ili kuruhusu misaada ya kuokoa maisha kuwafikia watu walioathirika huko El Fasher na kuonya kuwa wahusika wa vitendo hivyo vya kikatili watawajibishwa.”

“Baraza linaomba Tume ya AU kufuatilia mara kwa mara na kuripoti uhalifu huo wa kutisha unaofanywa kote nchini Sudan, ili kuweka hatua za kuzuia na kupunguza hatari ya kutokea tena; kuendeleza mapendekezo ya jinsi ya kushughulikia ili kuzuia kuongezeka kwao zaidi; kuunda mpango wa ulinzi wa raia, na kutoa mapendekezo kwa PSC ndani ya wiki tatu;

CHANZO:TRT Swahili