Maandamano Dar es Salaam huku Uchaguzi Mkuu ukiendelea Tanzania
Mamia ya raia wameandamana kuelekea Daraja la Salenda linaloelekea katikati mwa jiji la Dar es Salaam, Reuters imesema
Maandamano Dar es Salaam huku Uchaguzi Mkuu ukiendelea Tanzania
Uchaguzi Mkuu nchini Tanzania unafanyiak 29 Oktoba 2025 / Reuters
tokea masaa 10

Maandamano yaliripotiwa kuzuka katika mji mkuu wa kibiashara wa Tanzania, Dar es Salaam, Jumatano wakati wa Uchaguzi Mkuu.

Huduma ya mtandao ilitatizika kote nchini, Shirika linalofuatilia masuala ya mitandao NetBlocks lilisema, huku video, ambazo hazijathibitishwa bado, za waandamanaji vijana wakirusha mawe kwa maafisa wa usalama na kituo cha kuuza mafuta zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Mamia ya watu walikuwa wakiandamana kuelekea Daraja la Salenda linaloelekea katikati mwa jiji la Dar es Salaam, alisema mmoja ya walioshuhudia ambaye aliomba jina lake lisitajwe.

Walioshuhudia wanasema kumekuwa na vurugu katika mitaa ya Dar es Salaam, wakati vyombo vya habari vikionyesha polisi wakitumia mabomu ya machozi kuwatawanya waandamanaji katika sehemu nyingine za jiji.

Wasemaji wa serikali na polisi hawakujibu mara moja maombi ya kulizungumza suala hili, na Reuters haikuweza kuthibitisha uhakika wa video hizo kwenye mitandao ya kijamii.

Kura hiyo inafanyika bila ya ushiriki wa chama kikuu cha upinzani CHADEMA ambacho kiongozi wake Tundu Lissu anakabiliwa na kesi ya uhaini mashtaka ambayo amekuwa akikanusha.

Tume ya uchaguzi iliiondoa CHADEMA mwezi Aprili baada ya kukataa kutia saini kanuni ya maadili ya uchaguzi.

CHANZO:TRT Afrika and agencies