AFRIKA
1 dk kusoma
Uganda yazindua mkahawa nchini Saudi Arabia
Makamu wa Rais wa Uganda, Jessica Alupo, amezindua mkahawa wa Uganda nchini Saudi Arabia. Mkahawa unaofahamika kwa jina la Nonda, utakuwa na mfumo wa kuwa na misururu ya mikahawa kila mahali.
Uganda yazindua mkahawa nchini Saudi Arabia
Makamu wa rais wa Uganda, Jessica Alupo. / Reuters
tokea masaa 8

Mkahawa huo wa Nonda Coffee Shop, umezinduliwa katikati ya mji wa Riyadh na ni hatua muhimu ya kihistoria kwa kutangaza kahawa ya Uganda.

Hii ni mara ya kwanza kwa Uganda kufungua mkahawa wao wenyewe ambao utakuwa na mikahawa kama hiyo katika maeneo mbalimbali duniani. Kwa uwekezaji huu wakazi wa mataifa tofauti, wasafiri na mamilioni ya wageni kutoka sehemu nyingi wanaotembele Saudi Arabia watapata nafasi ya kufurahia kahawa ya Uganda, ikiwemo wale wanaokwenda Hijja na kutalii.

Hatua hii ni ya kwanza tu na inatarajiwa kuwa kutakuwa na mikahawa mingi kama hii kote nchini Saudi Arabia.  

Katika hotuba yake, Makamu wa Rais wa Uganda Jessica Alupo alisema uzinduzi wa Mkahawa wa Nonda nchini Saudi Arabia ni hatua muhimu kwa Uganda, wakati ikitafuta masoko mapya kwa ajili ya kahawa yake. Aliongeza kuwa hii haitokuwa kuuza kahawa tu, bali pia kutengeneza nafasi za ajira kwa raia wa Uganda na kuhamasisha wakulima wadogo wadogo kuimarisha uzalishaji wao kwa ajili ya biashara zaidi.

CHANZO:TRT Afrika Swahili