AFRIKA
1 dk kusoma
Kampeni za Uchaguzi Mkuu Tanzania kukamilika
Pazia la kampeni hatimae linafungwa nchini Tanzania, hii ikiashiria miezi miwili ya heka heka za wanasiasa kutoka vyama mbalimbali kuomba ridhaa ya wananchi Ili kupewa nafasi za uongozi katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.
Kampeni za Uchaguzi Mkuu Tanzania kukamilika
Moja ya kituo cha kupiga kura. / TRT Afrika
tokea masaa 14

Abubakar Famau akiwa Zanzibar

Kampeni hizo zilizodumu kwa kipindi cha miezi miwili zilitakiwa kutoa fursa sawa kwa vyama 18 vinavyoshiriki Uchaguzi Mkuu kunadi sera zake ili wapiga kura milioni 34 kufanya maamuzi sahihi ifikapo Oktoba 29.

Katika kampeni hizo, kuna ahadi mbalimbali zilizotolewa. Wapo walioahidi kuimarisha huduma za msingi kama vile afya, maji na miundombinu. Lakini wapo pia waliokwenda mbali zaidi na kuahidi mpaka kufuga mamba Ikulu kwa lengo la kupambana na rushwa na ufisadi.

Mumuhimu uamuzi sasa unabaki kwa wananchi wenyewe. Ndio watakaoamua kupitia sanduku la kura.
Kwa mujibu wa Tume Huru ya Uchaguzi nchini Tanzania maandalizi yote yamekamilika huku Zanzibar wakifungua dimba kwa kura za awali Oktoba 28 ambazo zinajumuisha watumishi wa umma.
Kwa mujibu wa Tume Huru ya Uchaguzi kuna jumla ya wagombea 34 wa urais na wagombea wenza wao kutoka vyama 17 vya kisiasa.
Wakati huo huo Tume hiyo imesema itatangaza mshindi wa mgombea urais ndani ya saa 72.

CHANZO:TRT Afrika