tokea masaa 2
Siku ya Ijumaa rais wa Madagascar amemfuta kazi waziri wake wa nishati kwa lengo la kutuliza maandamano kuhusu kukatwa kwa umeme mara kwa mara na uhaba wa maji, ambayo yamesababisha machafuko katika mjii mkuu siku moja kabla.
Polisi walitumia risasi za mpira na mabomu ya machozi kutawanya waandamanaji wengi wao wakiwa vijana katika mji wa Antananarivo siku ya Alhamisi, katika maandamano ambayo Rais Andry Rajoelina ameyaita "ya kutatiza nchi sawa na mapinduzi" katika kauli yake ya kwanza kwa njia ya video.
Zilizopendekezwa
Walioandaa maandamano siku ya Ijumaa walitaka watu ambao hawaridhiki na serikali ya Rajoelina "kujitokeza kwa wingi" kwa "maandamano ya amani" siku ya Jumamosi asubuhi, wakijitenga na matukio ya uporaji ya siku ya Alhamisi.
CHANZO:TRT Afrika Swahili