Abbas, ambaye ni kaka mkubwa wa Rais wa Zanzibar Hussein Ali Mwinyi, alifariki dunia Septemba 25, 2025, wakati akipokea matibabu katika hospitali ya Lumumba, iliyopo Mkoa wa Mjini Magharibi.
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi nchini Tanzania (INEC), imeahirisha uchaguzi wa kiti cha ubunge katika jimbo la Fuoni, kufuatia kifo cha mgombea wa jimbo hilo kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abbas Ali Mwinyi.
Abbas, ambaye ni kaka mkubwa wa Rais wa Zanzibar Hussein Ali Mwinyi, alifariki dunia Septemba 25, 2025, wakati akipokea matibabu katika hospitali ya Lumumba, iliyopo Mkoa wa Mjini Magharibi.
Taarifa iliyotolewa na Msimamzi wa Jimbo la Uchaguzi la Fuoni, Miraji Mwadini Haji, imesema kuwa taarifa za kifo cha mwanasiasa huyo, zilipatikana kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar.
INEC imesema itapanga tarehe nyingine ya uteuzi wa wagombea na taratibu za uchaguzi katika jimbo hilo zitaanza upya.
Abbas, ambaye pia ni rubani, anatarajiwa kuzikwa Septemba 26, 2025 katika eneo la Mangapwani.