AFRIKA
2 dk kusoma
Waziri mkuu wa Sudan aomba UN, jamii ya kimataifa kutangaza RSF kuwa ‘wapiganaji wa kigaidi’
Idris ameomba jamii ya kimataifa, Umoja wa Mataifa kuzuia kufikishwa kwa silaha, na mamluki ndani ya nchi
Waziri mkuu wa Sudan aomba UN, jamii ya kimataifa kutangaza RSF kuwa ‘wapiganaji wa kigaidi’
Sudan
tokea masaa 7

Waziri Mkuu wa Sudan Kamil Idris siku ya Alhamisi alitoa wito kwa jamii ya kimataifa na Umoja wa Mataifa kulitaja kundi la wapiganaji wa RSF kama “wapiganaji wa kigaidi.”

Katika hotuba wakati wa kikao cha 80 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York, Idris aliomba jamii ya kimataifa na Umoja wa Mataifa kuzuia kuingizwa kwa silaha na mamluki nchini Sudan.

Amesema “watu wa Sudan wamepata vitisho na hatari kubwa kwa sababu ya RSF, ambao wamekuwa na sera ya kushambulia raia.”

Tangu Aprili 2023, jeshi la Sudan la RSF wamekuwa wakipigana katika vita vya wenyewe kwa wenyewe na kusababisha mauaji ya maelfu ya watu na mamilioni wengine kuhama makazi yao.

Idris alitoa wito wa kusitishwa kwa kuzuiwa kwa watu katika mji wa El-Fasher, ikiwa sanjari na maamuzi ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Alishtumu kuendelea kukaa kimya kwa jamii ya kimataifa kuhusu hali hiyo na kushambuliwa kwa kambi za walioondolewa kwenye makazi yao, miskiti, na huduma za afya kote nchini.

Kumekuwa na mapigano makali El-Fasher kati ya jeshi na RSF tangu Mei 2024, licha ya jamii ya kimataifa kuonya kuhusu hatari ya mapigano katika mji huo ambao ndiyo kituo kikuu cha misaada kwa majimbo yote matano ya Darfur.

Idris pia aligusia kuhusu hali mbaya kwa watu katika ukanda wa Gaza, akisema kuwa ‘‘ni hatari kubwa kwa kanda hiyo na watu wake.”

“Hakutakuwa na uthabiti na usalama katika kanda bila suluhu kamili ya suala la Palestina, na kuwezesha kuundwa kwa taifa la Palestina huku Jerusalem ikiwa makao makuu yake kulingana na mipaka ya 1967,” alisema.

Idris alishtumu mashambulizi ya hivi karibuni ya Israel kwa uongozi wa Hamas huko Doha, Qatar, akisema inatishia amani na usalama wa kimataifa.

CHANZO:AA