Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi nchini Tanzania (INEC) imetoa takwimu mpya za wapiga kura waliojiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Oktoba 7, INEC imesema kuwa mabadiko hayo ni kutokana na mabadiliko ya takwimu za wapiga kura na idadi ya vituo vya kupigia kura yaliyowasilishwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar.
"Jumla ya wapiga kura waliopo katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura la Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 ni 37,647,235 badala ya 37,655,559 iliyotangazwa hapo awali," imesema taarifa ya Tume.
Tume hiyo pia imeongeza kusema kuwa, idadi hiyo ya wapiga kura ni sawa na ongezeko la asilimia 26.53 kutoka idadi ya wapiga kura 29,754,699 waliokuwa katika Daftari la Wapiga Kura mwaka 2020.












