30 Septemba 2025
Mahakama ya kijeshi nchini DRC imetoa hukumu ya kifo kwa Rais wa zamani wa nchi hiyo, Joseph Kabila baada ya kumkuta na hatia ya uhalifu wa kivita.
Kulingana na Luteni Jenerali Joseph Mutombo, kiongozi huyo wa zamani alipatikana na hatia mbalimbali, ikiwemo uhaini, unyanyasaji wa kingono, mauaji na uhalifu dhidi ya binadamu.
Hata hivyo, Kabila hakuwepo mahakamani wakati wa kutolewa kwa hukumu hiyo, siku ya Jumanne jijini Kinshasa.
Kabila, ambaye aliiongoza Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kutoka mwaka 2001 hadi 2019, amepinga hukumu hiyo, akisisitiza kuwa mahakama ya nchi hiyo ‘imehadaiwa’ kisiasa.
Aliondoka madarakani kufuatia vurugu za kisiasa zilizotokea nchini humo, na amekuwa akiishi Afrika Kusini toka mwishoni mwa mwaka 2023.
CHANZO:Reuters