Vikosi vya usalama vilifyatua mabomu ya machozi kuwatawanya mamia ya waandamanaji vijana katika mji mkuu wa Madagascar ambao waliingia tena mitaani siku ya Jumanne licha ya uamuzi wa rais wa kuitikia matakwa yao kwa kuvunja serikali.
Andry Rajoelina alienda kwenye runinga ya serikali mwishoni mwa Jumatatu na kusema anataka kuunda nafasi ya mazungumzo na vijana wanaoshinikiza kupata maji na kukomesha kukatwa kwa umeme, na kuahidi hatua za kusaidia biashara zilizoathiriwa na uporaji.
Katika ujumbe kwenye ukurasa wa Facebook wa vuguvugu hilo la maandamano, baadhi ya waandalizi wa maandamano hayo walisema wamesikitishwa na hotuba yake huku wakitaka kuombwa radhi kutoka kwake na kwa waziri mkuu aliyefukuzwa kazi, pamoja na kufutwa kazi kwa msimamizi wa Antananarivo.
Wengine walikwenda mbali zaidi, wakipeperusha mabango yenye ujumbe kama vile "Tunahitaji maji, tunahitaji umeme, Rajoelina nje", picha za waandamanaji wakiandamana katika mji mkuu wa Antananarivo, zilizotangazwa kwenye kituo cha utangazaji cha kibinafsi cha Real TV Madagasikara.
Takriban watu 22 wamefariki
Maandamano pia yalifanyika katika mji wa Fenoarivo, mji mdogo ulio kilomita 20 (maili 12) magharibi mwa mji mkuu, kanda za video kutoka Real TV zilionyesha.
Mikutano ya hadhara iliripotiwa huko Mahajanga, kilomita 510 (maili 315) kaskazini-magharibi mwa Antananarivo, na huko Diego Suarez, kilomita 950 kaskazini mwa mji mkuu, 2424.MG inayomilikiwa kibinafsi na Fitaproduction iliripoti.
Msemaji wa serikali hakujibu mara moja ombi la maoni juu ya maandamano ya Jumanne. Umoja wa Mataifa unasema takriban watu 22 wameuawa na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa katika maandamano yaliyoanza wiki iliyopita na sasa ni siku ya nne.
Wizara ya mashauri ya nchi za kigeni imekataa takwimu za majeruhi zilizoshirikiwa na Umoja wa Mataifa, ikisema data hizo hazikutoka kwa mamlaka ya kitaifa yenye uwezo na zilitokana na uvumi au habari potofu.